Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika na serikali ya Sudan wakutana Ethiopia

Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika na serikali ya Sudan wakutana Ethiopia

Maafisa kutoka Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa na serikali ya Sudan leo wanakutana mjini Addis Ababa Ethiopia .

Katika mkutano wao wa nane wa pande tatu watajadili suala la vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na wa Afrika UNAMID, jinsi ya kuvilinda vikosi hivyo na jukumu lake nchini Sudan.

Majadiliano ya pande hizo tatu yalianzishwa Mwezi Julai mwaka 2008 Sharm El Sheikh nchini Misri kwa minajili ya kuchagiza juhudi za kupelekwa wanajeshi wa ziada wa kulinda amani pamoja na kuimarisha uhusiano mwema kati ya serikali ya Sudan na vikosi hivyo.

Na tangu kufanyika kwa mkutano wa kwanza wa pande hizo tatu kumekuwepo na fursa nzuri ya ushirikiano kwa manufaa ya watu wa jimbo la Darfur.