Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malezi bora kwa watoto wachanga muhimu katika kutimiza malengo ya milenia

Malezi bora kwa watoto wachanga muhimu katika kutimiza malengo ya milenia

Takwimu za mwaka 2010 zilizotolewa leo na shirika la afya duniani WHO zinasema kuimarisha malezi ya mtoto mchanga katika mwezi wa kwanza wa maisha yake ni muhimu sana katika kupunguza vifo vya watoto kwenye nchi zinazoendelea.

Takwimu hizi zimetolewana WHO katika kuangalia maendeleo ya kutaka kufikia malengo ya milenia (MDG'S). Duniani kote asilimia 40 ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano vinakadiriwa kutokea katika mwezi wa kwanza wa uhai wao na vingine katika wiki ya kwanza.

WHO inasema juhudi kubwa zinahitajika ili kuimarisha malezi na huduma muhimu kwa watoto hususani kwenye wiki za kwanza za uhai wao ili kuweza kufikia malengo ya milenia ya kupunguza vifo vya watoto wachanga. Carla Abou-Zahr ni mratibu WHO