Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo baina ya Israel na Palestina ni mwanzo wa matumaini ya amani :UM

Mazungumzo baina ya Israel na Palestina ni mwanzo wa matumaini ya amani :UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ametiwa moyo na kuanza kwa mazungumzo ya awali baina ya Israel na Palestina.

Amesema hatua hiyo inaleta matumaini kwamba hatimaye itachagiza kuwepo kwa majadiliano ya moja kwa moja baina ya pande hizo mbili. Kwa mujibu wa duru za habari ,ilitangazwa jana kuwa mazungumzo ambayo si ya moja kwa moja yanayosimamiwa na Marekani yameanza kati ya Israel na Palestina. Katika taarifa yale iliyotolewa na msemaji wake Bwana Ban amepongeza juhudi za Marekani na kuelezea matuimaini kuwa hatua zitapigwa katika mchakato wa amani.

Nalo shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP katika ripoti yake mwishoni mwa wiki linasema hadi pale Wapalestina watakapoweza kuwa na udhibiti wa sera za maendeleo, biashara, maisha, rasilimali kama maji na udhibiti wa mipaka, maendeleo endelevu yatasalia kuwa ndoto tu.