Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa WFP kushiriki mkutano wa chakula unaohusisha Brazili na Afrika

Mkuu wa WFP kushiriki mkutano wa chakula unaohusisha Brazili na Afrika

Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani Josette Sheeran anaanza ziara ya siku mbili nchini Brazili mwishoni mwa wiki kushiriki mkutano wa usalama wa chakula to baina ya Brazil na Afrika .

Mawaziri wa kilimo kutoka barani Afrika watahudhuria mkutano huo unaoanza Jumatatu ijayo. WFP inasema Brazil imekuwa ikichukuwa jukumu la kusaidia masula ya kibinadamu , ikiwa ni pamoja na kushirikisha wengine ,katika operesheni za programu zake.

Bi Sheeran atakutana na Rais Luis Inácio Lula da Silva na viongozi wengine wa serikali ya Brazil. Atamkabidhi Rais Lula tuzo ya kimataifa ya kuwa kinara katika vita dhidi ya njaa ijulikanayo kama "Global Champion in the Battle Against Hunger". WFP imebaini kuwa Brazil inasaidia mpango wa kutoa mlo mashulen Amerika ya Kusini na Afrika mpango ambao unawapa watoto lishe bora ambayo ni msingi wa maisha yao ya baadaye.