Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Holems aelezea matatizo yaliyosababishwa na ukame Niger na vita DR Congo

Holems aelezea matatizo yaliyosababishwa na ukame Niger na vita DR Congo

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema bado dunia ina fursa ya kunusuru janga la njaa nchini Niger ambako watu karibu nusu wamekumbwa na ukame.

John Holems aliyekuwa ziarani Niger na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hivi karibuni amesema Congo pia inahitaji msaada muhimu wa kibinadamu baada ya kusambaratishwa na vita. Amesema la sivyo nchi hiyo itaathirika vibaya na kuondoka mapema kwa vikosi vya kulunda amani vya Umoja wa Mtaifa nchini humo MONUC.

Akizungumza hapa New York baada ya kurejea kutoka katika nchi hizo mbili Holmes amesisitiza haja ya wahisani kuingilia kati na kusaidia kwa Niger inayohitaji dola zaidi milioni 130 mbali ya mdola milioni 70 ambazo zimekwisha pokelewa ili kuwalisha watu milioni 7.8 wanaokabiliwa na njaa.Na kwa Congo ambako misaada ya kibinadamu ina upungufu wa asilimia 73 na serikali imeomba kuondoka kwa vikosi vya MONUC ifikapo 2011.

Amesema jumuiya ya kimataifa iko katika nafasi nzuri ya kusaidia kabla hali haijawa mbaya zaidi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi kama ilivyokuwa mwaka 2005 kwa sababu taarifa ya tahadhari imeshatolewa mapema tofauti na mwaka 2005.