Afisa wa UM ataka makundi yenye silaha kukiachilia huru kituo cha afya Somalia

Afisa wa UM ataka makundi yenye silaha kukiachilia huru kituo cha afya Somalia

Afisa wa masuala ya misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Mark Bowden,ameyatolea wito makundi ya watu wenye silaha kuondoka katika kituo cha afya wanachokishikilia mjini Afgooye Somalia.

Makundi hayo ymekidhibiti kituo cha afya cha Hawa Abdi ambacho kimekuwa kikitoa huduma kwa wakimbizi wa ndani na wanaohitaji msaada tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990.Afisa huyo amesema Mark Bowen amesema wagonjwa ilibidi wahamishwe na makundi hayo yenye silaha yanamshikilia mkurugenzi wa kituo hicho cha afya.

Mark Bowden amesisitiza kwamba moja ya taratibu muhimu katika sheruia za vita ni kutoshambulia taasisi za afya ambazo zinajulikana waziwazi au wahudumu wa afya ambao wanatoa msaada kwa watu wengine wanaohitaji huduma.

Ametatolea witio makundi hayo yenye silaha ambayo khazia zake zimeingilia shughuli za kituo hicho cha afya ,na amewataka waweke silaha chini na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwasili na kuanza tena huduma za kituo hicho. Kuna wakimbizi wa ndani zaidi ya 350,000 kwenye makambi ya muda kwenye eneo la kilometa 13 kati ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu na Afgooye.