Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa shirika la UM la haki za binadamu atazuru Asia Mashariki

Mkuu wa shirika la UM la haki za binadamu atazuru Asia Mashariki

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Navi Pillay atahutubia mkusanyiko mkubwa wa kimataifa wa wanawake majaji wakati wa ziara yake Asia Mashariki itakayojumuisha Jamhuri ya watu wa Korea na Japan.

Bi Pillay atakuwa mzungumzaji mkubwa kwenye mkutano wa kumi wa kimataifa wa jumuiya ya majaji wanawake utakaoanza May 12 mjini Seol.Atakapokuwa katika mji mkuu huo wa korea Bi Pillay atakutana pia na kaimu waziri wa mambo ya nje na biashara ChunYoung-Woo.

Baada ya hapo atakwenda Japan May 13 kuwa na mazungumzo na waziri mkuu Yukio Hatoyama, wazoieri wa mambo ya nje Katsuya Okada na waziri wa sheria Keiko Chiba.

Akiwa mjini Tokyo Bi Pillay atakutana na viongozi wa serikali, wabunge, na wawakilishi wa jumuiya za kiraia , na makundi ya walio wachache na pia familia za watu waliotekwa Korea Kaskazini.