Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF imeelezea hofu yake kwa kuwatumia watoto kwenye maandamano Nepal

UNICEF imeelezea hofu yake kwa kuwatumia watoto kwenye maandamano Nepal

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa watoto UNICEF limesema kuna wasiwasi kuwa chama kinachofuata siasa za Kimao nchini Nepal kinawatumia watoto katika maandamano ynayoendelea nchini humo.

Shirika hilo limesema kuna ripoti zilizothibitishwa kuwa watoto wengi walihudhuria maandamano.Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF Christiane Berthiaume, shirika lake lina hofu kuwa kutakuwa na maandamano ya kupingana na watoto watashirikishwa.

(CLIP CHRISTIANE)

Wakati huo huo UNICEF inasema kufungwa kwa shule wakati wa muda wa maandamano ni ukiukaji wa haki ya watoto ya masomo.