Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wahamishiwa Moula Chad

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wahamishiwa Moula Chad

Wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR walioko kusini mwa Chad wameanza shughuli ya kuwahamisha wakimbizi 1,100 wapya waliowasili kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wakimbizi hao wanapelekwa kwenye kambi ya Moula ambako watapewa msaada unaohitajika. Watu hao walikimbia mapigano katika eneo la Sido, Kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kukimbilia mkoa wa Moyen unaopakana na Chad wiki mbili zilizopita.

Jeshi la serikali na waasi wamekuwa wakipambana katika eneo hilo la Sido. Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR wanawasafirisha wakimbizi hao hadi kambi ya Moula iliyoko kilometa 180 kusini magharibi. Kufikia jana walikuwa wameshawasafirisha wakimbizi 204 na wanapanga kukamilisha shughuli hiyo mapema wiki ijayo.