Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa la uchumi limemalizika nchini Tanzania:Tibaijuka

Kongamano la kimataifa la uchumi limemalizika nchini Tanzania:Tibaijuka

Kongamano la kimataifa la uchumi kwa ajili ya maendeleo barani Afrika limemalizika leo Dar es salaam nchini Tanzania.

Kongamano hilo lilijumuisha wakuu wan chi zaidi ya kumi, wawakilishi kutoka nchi 85 duniani, wawekezaji, wafanya biashara, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali.Ajenda mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo suala la kilimo, elimu, uwekezaji, demokrasia na ukombozi wa mwanamke.

Miongoni mwa wazungumzaji katika kongamano hilo ni Dr Anna Tibaijuka nkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT na anafafanua jukumu la Umoja wa Mataifa kwenye mkutano huo