Mwalishi wa UM nchini Afghanistan alaani mashambulizi dhidi ya majengo ya serikali

6 Mei 2010

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Matafa nchini Afghanistan Staffan de Mistura leo amelaani mashambulizi dhidi ya majengo ya serikali katika eneo la Kusini Magharibi mwa nchi hiyo ambayo ametaja kama ya kusikitisha.

Duru zinasema , Gul Makai Wakil, mwanacham wa serikali ya kimkoa pamoja na maafisa watatu waliuwawa katika shambulizi hilo ambalo lilijibizwa na wanajeshi na polisi wa Afghanistan katika eneo la Zaranj, mjii mkuu wa mkoa wa Nimroz. Raia wanne na maafisa saba walijeruhiwa katika tukio hilo.

Bi Gul Makai ambaye ni mtunzi wa mashairi , amekuwa msitari wa mbele kupigania haki za akina mama mjini Zaranj, anaheshimiwa na wakaazi wa eneo lake kwa kuwa na mtazamo wa kitaifa kwa Afghanistan.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter