Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa mataifa kusaidia mapambano dhidi ya surua nchini Zimbabwe

Umoja wa mataifa kusaidia mapambano dhidi ya surua nchini Zimbabwe

Takribani watoto milioni tano nchini Zimbabwe watapokea kinga inayohitajika dhidi ya ugonjwa wa surua kutokana na fedha zilizotolewa na fungu la dharura la Umoja wa Mataifa.

Licha ya watoto 48,000 kuchanjwa katika wilaya 23 mlipuko wa surua mwezi Septemba mwaka jana umeongeza maambukizi ya ugonjwa huko kwa watu wapya 6,200 na idadi ya watoto waliofariki dunia imefikia 384 katika wilaya 57 kati ya 62 za nchi hiyo.

Mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa John Holemes amesema fedha hizo zitasaidia katika mpango wa haraka wa chanjo kwa watoto dhidi ya surua ugonjwa ambao unaweza kuzuilika.