Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya misaada yahofia usalama Chad vikiondoka vikosi vya kulinda amani

Mashirika ya misaada yahofia usalama Chad vikiondoka vikosi vya kulinda amani

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yameelezea hofu yake juu ya tishio la usalama nchini Chad kufuatia kuanza kuondoka kwa hatua vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.

Mashirika hayo yanasema hofu yao hasa ni juu ya operesheni zake nchini humo hasa kuwagawia misaada muhimu maelfu ya watu wanaoihitaji. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kesho litaamua hatima ya kuondoa vikosi vyake vya kulinda amani nchini humo MINUCART kufuatia ombi la serikali ya Chad mwezi Januari.

Hata hivyo shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA leo wameambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa ongezeko la unyang'anyi na mashambulizi dhidhi ya magari ya misaada imekuwa kikwazo cha wao kuwafikia watu wanaohitaji msaada.

(SAUTI WFP: Tunakimbizana na muda ili kuwasilisha chakula kwa muda kabla ya kuanza msimu wa mvua ambao ni karibuni. Tumepokea asilimia 55 ya fedha zinazohitajika, tunahitaji fedha zaidi na tunazika sasa hivi ili tuweze kununua chakula sasa, ili kuwe na nafasi ya kukipokea wakati wa August na Septemba, ili kukamilisha mipango ambayo tumeshaiweka mpaka mwishoni mwa mwaka huu.)