Skip to main content

Upungufu wa chakula barani Afrika unahitaji suluhu haraka:Diouf

Upungufu wa chakula barani Afrika unahitaji suluhu haraka:Diouf

Mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jacques Diouf ametoa wito wa kulishughulikia kwa haraka tatizo la upungufu wa chakula barani Afrika.

Akizungumza kwenye mkutano wa 26 wa FAO kwa ajili ya Afrika mjini Luanda Angola amesema katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara tangu mwaka 2009 watu zaidi ya milioni 260 wameathirika kiafya kwa kukosa chakula na asilimia 30 wanakabiliwa na njaa.

Ameongeza kuwa hali hii inahitaji kuangaliwa na kushughuliwa kwa haraka, akinukuu kwamba licha ya athari za msukosuko wa kiuchumi duniani lakini bado kilimo ndio nguzo ya maendeleo ya mataifa mengi, na kutangaza kuwa hatua mpya zitatoa fursa ya kuwasaidia wakulima wadogowadogo na kuimarisha kilimo katika ngazi ya familia. Kilimo barani Afrika kinakabiliwa na vikwazo vingi ikiwepo ukosefu wa maji na vifaa pia miundombunu mibovu vijijini.