5 Mei 2010
Baraza la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili kuhusu shughuli ya Umoja wa Mataifa katika kuisaidia jitihada za kupatikana kwa amani nchini NEPAL, baada ya makundi hasimu kukosa kuafikiana kuhusu maswala muhimu ya ugavi wa mamlaka na katiba mpya.
Baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2008, Nepal, ilifutilia mbali utawala wa kifalme wa miaka mia mbili na arobaini na kujitangaza kama jamhuri. Lakini juhudi za amani zimekwama baada ya ukosefu wa imani kati ya serikali, wanajeshi na kundi la Kimao
bahari ya Hindi.