Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Kisomali kunufaika na mradi wa maji na umeme :UNHCR

Wakimbizi wa Kisomali kunufaika na mradi wa maji na umeme :UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limemalizisha mradi

utakaogharimu mamilioni ya dola wa umeme na maji ambao utawanufaisha maelfu ya watu wakiwemo wakimbizi wa kutoka Somalia na baadhi ya jamii ya wakaazi katika eneo kame mashriki mwa Ethiopia.

Mradi huo wa maji ya bonde la Jarar uliogharimu dola milioni tano katika eneo linalokaliwa na Wasomali nchini Ethiopia utasambaza maji safi lita milioni 1.3 kila siku kwa watu 51,000 wakiwemo wakimbizi 16,000 kwa kutumia umeme

Mradi huo ulianzishwa mwezi uliopita na naibu kamishana wa wakimbizi Alexander Aleinikoff, na mpango wa kuwapa watu laki moja maji wakati wa msimu wa ukame.