Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwema wa UNICEF apigia chepuo afya ya mama na mtoto Guinea

Balozi mwema wa UNICEF apigia chepuo afya ya mama na mtoto Guinea

Mwigizaji maarufu na balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Mia Farrow anakwenda nchini Guinea kutoa msukumo wa juhudi za kulinda afya ya mama na mtoto.

Juhudi hizo ni pamoja na kuchangisha fedha ili kuisaidia nchi hiyo ambayo vijana wengi wameathirika na mzozo wa kisiasa wa hivi karibuni.

Ongezeko la maambukizi ya magonjwa kwa watoto, pia idadi kuwa ya watoto kuacha shule ni ishara kwamba kutakuwa na hali mbaya katika siku zijazo endapo ufumbuzi hautopatikana ameonya mkuu wa shirika la UNICEF nchini Guinea.

Ameongeza kuwa hatma ya watoto nchini humo ngumu mno iwapo hakutakuwa na uwekezaji na juhudi kubwa ili kukabiliana na mahitaji yao.