Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ametangaza hatua mpya za mpango wa kulinda amani MINUCART

Ban ametangaza hatua mpya za mpango wa kulinda amani MINUCART

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea mapendekezo yake kuhusu mpango mpya wa wanajeshi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad MINURCAT.

Katika ripoti yake kuhusu mataifa hayo Katibu Mkuu Ban amesema idadi ya wanajeshi wa kulinda amani itapunguzwa kwa kiasi kikubwa nah ii inafuatia maombi ya nchi ya Chad ya kuchukua jukumu la kuwalinda raia wake.

Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa na serikali ya Chad walikubaliana kupunguza idadi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ambapo baadaye serikali ya Chad imeomba kuondolewa kwa kitengo cha MINURCAT ikisema kimeshatimiza wajibu wake.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kuanzishwa kwa MINURCAT miaka miwili iliyopita na muda wake ulikuwa unakwisha tarehe 15 mwezi huu wa May.