Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa la uchumi limeanza leo nchini Tanzania

Kongamano la kimataifa la uchumi limeanza leo nchini Tanzania

Kongamano hilo linaangazia zaidi maswala yanayoikabili Afrika kauli mbiu ikiwa kufikiria upya ukuaji wa maendeleo barani Afrika, na linafanyika jijini Dar es salaam.

Kongamano hilo linashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Jumla ya marais 11 wa kutoka barani Afrika wanahururia pamoja na wajumbe wengine kutoka nchi 85 duniani watakuwa nchini humo kwa siku tatu. Umoja wa Mataifa unawakilishwa na mashirika na watu mbalimbali akiwemo naibu Katibu Mkuu Dr Asha Rose Migiro na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT Dr Anna Tibaijuka.

Clement Mshana ni mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ya Tanzania na ni miongoni mwa waratibu wa kongamano hilo anafanua ajenda kuu za mkutano