Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani inasema opokonyaji silaha na udhibiti ni hakikisho la usalama:NTP

Ujerumani inasema opokonyaji silaha na udhibiti ni hakikisho la usalama:NTP

Ushirikiano wa kimataifa unahitajika kuhakikisha silaha za nyuklia zinatokemezwa duniani na kuwahakikishia watu usalama.

Huo ni ujumbe uliotolewa na mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kimataifa wa tathmini ya kupunguza silaha za nyuklia duniani NTP kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York unaoingia siku yake ya tatu.

Wakati wa mjadala masuala yaliyojitokeza ni pamoja na ubaguzi wa kupata fursa ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya raia, uzalishaji wa zana za nyuklia, jinsi ya kujivua silaha hizo, kutekeleza mkataba wa kupinga nyuiklia na matumizi ya amani ya nyuklia. Ujerumani imeutaka mkutano huo kutoa ujumbe mzito wa ushirikiano kwamba nchi zote zinahitaji ushirikiano zaidi katika kudhibitii silaha na kupunguza idadi ya silaha wanazomiliki.