Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa fedha umeifanya WFP kupunguza mgao wa chakula Yemen

Upungufu wa fedha umeifanya WFP kupunguza mgao wa chakula Yemen

Ukosefu wa fedaha umelilazimu shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kupunguza kwa nusu kiwango cha chakula cha msaada kwa watu wa Yemen, kwanzia mwezi huu.

WFP inasema nusu ya chakula cha msaada watapewa hususan watu takriban laki mbili na elfu sabini ambao wameaachwa bila makao kufuatia mapigano katika eneo la Sa'ada. Wengi wao ni watoto wenye umri wa chini ya miaka tano na akina mama wajawazito. Msemaji wa WFP Emilia Casella ameonya kuwa ifikapo mwezi wa Agosti mwaka huu WFP itakuwa imemaliza chakula cha akiba, kikiwemo chakula cha kuwasaaidia watu nusu millioni ambao ni wakimbizi wa ndani.

(LIP CASELLA:Tunaona watoto walio na umri wa mwaka moja wakiwasili katika maeneo ya kupewa chakula wakiwa na uzito na urefu ya watoto waliozaliwa hivi majuzi. Na tunaona familia ambayo inakula mkate na chai siku nzima. Pengine wanakuwa mboga wakati mwingine katika wiki moja lakini hawapati nyama,samaki, mayai, vyakula vinavyompa mtu protini na vitamini ambavyo ni muhimu sana kwa afya )