Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Mameya kuhusu amani umeanza kwenye makao makuu ya UM

Mkutano wa Mameya kuhusu amani umeanza kwenye makao makuu ya UM

Baadhi ya manusura wa maafa ya bomu la Atomiki ni washiriki katika mkutano wa Mameya kwa ajili ya amani ulioanza hivi leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Mkutano huu unaendelea sambabmba na ule ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa kuhusu kusamba kwa zana za nyuklia, yaani NPT. Katika hotuba yake ya ufunguzi ya mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejea wito wake wa kusimamisha kusambaa kwa zana za nyuklia.

(CLIP BAN:Kadri mtu anavyoangalia kwa makini athari kwa kibinadamu, za kiuchumi na za kimazingira kwa uvamizi wa nyuklia au ajali yake, ndivyo inavyokuwa bayana ni lazima tusimamishe usambazaji wa nyuklia. Mkutano wa mwaka 2000 wa NPT unaweka wazi wazi kwamba kuangamizwa kwa zana za nyuklia ni hakikisho la kipekee dhidhi ya utumiaji au tishio la kutumia nyuklia)

Mkutano huo wa mameya kwa ajili ya amani unawajumuisha zaidi ya Meya 4000 na maafisa wa serikali wanaowakilisha watu karibu bilioni moja duniani. Meya wa Nagasaki na Heroshima, miji miwili ambayo iliangamizwa na bomu la atomiki mwaka wa 1945, wanahudhuria mkutano huo pamoja na manusura wa uvamizi huo wanaojulikana kama hibakusha.

Wkati huo huo, Ban ametangaza kuwa athudhuria hafla ya kumbukumbu ya amani ya Heroshima ya mwaka huu ambayo itafnyika mwezi wa Agosti na hivyo kumfanya yeye kama katibu Mkuu wa kwanza kuhudhuria hafla hiyo.

(CLIP BAN:Na hishi kuwa ni jukumu langu kwa mamia ya maelfu ya watu walio kufa au kujeruhiwa na uvamizi huo. Na nahisi jukumu sawia kwa vizazi vijavyo. Na nataka kusaidia juhudi ya kusimamisha usambazaji wa nyuklia ili mtu yeyote asiwe na hofu ya uvamizi wa nyuklia)