Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la JEM limejitoa kwenye mazungumzo ya amani ya Sudan

Kundi la JEM limejitoa kwenye mazungumzo ya amani ya Sudan

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID umearifu kwambva mapigano ya hivi karibuni baina ya kundi la Justice and Equality Movement (JEM) na serikali ya Sudan imethibitika kuwa yamesababisha vifo na watu wengi kukimbia nyumba zao.

UNAMID umezitaka pande zote kusitisha mapigano na kutotumia nguvu bali kutafuta suluhu kwa njia ya kisiasa wakitumia makubaliano ya amani yaliyopo baiana ya JEM na serikali. Msemaji wa JEM ametoa taarifa ya wao kujitoa kwenye mazungumzo ya amani kwa sasa yanayofanyika Doha Qatar. UNAMID inasema inaamini kuwa kujitoa huko kwenye mazungumzo ni kwa muda , wakisubiri suluhisho la masuala muhimu na inaamini mazungumzo hayo yatarejea tena.

Wapatanishi wanaendelea kuzungumza na kundi la JEM ili kuelewa wasiwasi wao na kushughulia , na wamelitaka kundi hilo kuendelea kuzingatia makataba wa kusitisha vita na kukamilisha mazungumzo ya amani na serikali na pia mkataba.