Skip to main content

FAO imeonya juu ya tishio la mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika

FAO imeonya juu ya tishio la mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limeonya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri juhudi za kupunmguza umasikini na upungufu wa chakula barani Afrika.

Onyo hilo limetolewa kwenye mkutano ulioandaliwa na FAo kwa ajili ya Afrika mjili Luanda Angola. Onyo hilo linasema matokeo ya ongezeko la joto na hali ya hewa isiyotabirika itapunguza mazao muhimu yanayotegemewa kama mahindi kwa asilimia 6.5.

Taarifa ya FAO pia inaelezea kwamba theluthi moja ya idadi ya watu barani Afrika wanaishi katika maeneo yenye ukame. Miji sita kati ya kumi mikubwa barani afrika iko katika ukanda wa pwani, na ni maeneo ambayo huathirika na mabadiliko ya hali ya hewa.