Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Iran kurejesha imani ya kimataifa kuhusu mipango yake ya nyuklia

Ban aitaka Iran kurejesha imani ya kimataifa kuhusu mipango yake ya nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinajad kurejesha imani ya kimataifa kuhusu mipango yake ya nyuklia.

Mipango ambayo Iran inasema ni ya amani, ametaka Iran ifanye hivyo kwa kuzingatia azimio la baraza la usalama na matakwa ya shirika la uchunguzi wa nyuklia la Umoja wa Mataifa. Katika mkutano wao hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Ban ametaka yaanze mazungumzo baiana ya Iran na nchi za pande sita ambazo ni Uchina, Ufaransa, Ujerumani, Urusi, Uingereza na Marekani kwa lengo la kutatua utata wa mipango ya Iran ya nyuklia ambayo baadhi ya nchi zinadhani ni ya kutengezeza silaha.

Iran inasema mipango yake ni ya amani na ni kwa ajili ya nishati, lakini bwana Ban akizungumza kwenye mkutano wa NTP amesema ni juu ya Iran kuhakikisha inafanya juhudi za kutatua utata uliopo.