Ba amezitaka nchi kuchukua hatua kukabliana na tishio la nyuklia

Ba amezitaka nchi kuchukua hatua kukabliana na tishio la nyuklia

Onyo kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu nyuklia ni kwamba ichukue hatua madhubuti, za kishujaa na za uongozi imara kukabiliana na tishio la nyuklia au iache wosia wa woga na kutowajibika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyasema hayo leo na ameuambia mkutano wa tathimini ya mkataba wa kuachana na silaha za nyuklia NTP ambao ni moja ya maazimio muhimu katika historia. Amesisitiza kuwa "Tunahitaji utawala huu kwa sababu tishio la nyuklia ni bayana na liko katika mifumo mbalimbali.

Na ndio maana mko hapa, watu katika dunia hii wanahitaji uwajibikaji wetu katika swala hili, hatua zaidi katika upokonyaji silaha, kupunguza silaha kabisa na kuwa wawazi. Kuna tofauti baiana ya walio na nyuklia na wasio nayo. Kuna hofu ya mauti na ongezeko la kuwa na ugaidi wa kutumia nyuklia, hasa kwenye masoko haramu ya teknolojia ya nyuklia na vifaa ambavyo ni vya hatari.

Ban ameonya kwamba suluhisho kwa changamoto zinazoukabili mkataba wa nyukila haziko katika moja ya mihimili mitatu. Amesema hatua katika kuachana na nyuklia haziwezi kusubiri dunia huru isiyo, uzalishaji wa nyuklia au ugaidi .Hatua haziwezi kusubiri kutokomezwa kwa silaha ya mwisho ya nyuklia. Na maendeleo ya matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia hayawezi kutiwa kitanzi ama kwa kulazimishwa kuachana nayo au kutozalisha kabisa.