Maonesho ya kimataifa ymefunguliwa Shangai, UM unashiriki

3 Mei 2010

Maonesho ya kimataifa ya Shangai yajulikanayo kama Shangai expo 2010 ymefunguliwa raismi na Rais wa Uchina Hu Jintao.

Katika maonyesho yaho mashirika 40 ya Umoja wa mataifa yanashiriki kuwakishilisha lengo moja la Umoja wa Mataifa. Na lengo hilo ni kuhakikisha dunia inaungana pamoja kuwa na maisha bora, elimu, afya, maendeleo, ukuaji wa miji na kuendeleza amani na usalama.

Ufunguzi wa maonesho hayo uliambatana na nderemo, vifijo na mafataki.

Kwa mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanasema hakuna uwezekano wa kuishi na kuwa na furaha kama kuna mmoja anajaribu kuharibu furaha hiyo, kwa kuchafua mazingira. Kila mmoja ana jukumu katika dunia hii kama ulivyo Umoja wa Mataifa, kuhakikisha dunia inakuwa mahala bora pa kuishi.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter