Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji tisa wa Kiafrika wapata hifadhi ya muda nchini Italia

Wahamiaji tisa wa Kiafrika wapata hifadhi ya muda nchini Italia

Wahamiaji tisa kutoka Afrika ambao wamekuwa wakinyonywa na kudhulimiwa na waajiri wao nchini Italia wamepewa kibali cha muda cha kukaa nchini humo chini kwa mujibu wa sheria za uhamiaji za Italia.

Wahamiaji hao wamefaidia na ushauri kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) kufiatia machafuko ya karibuni ya kupinga wahamiaji mjini Rosarno. IOM inasema hao tisa ni miongoni mwa mamia ya Waafrika wahamiaji ambao wengi wao wanatoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na wamekuwa wakifanya kazi kwenye mashamba kwa hadi saa 12 kwa siku na kulipwa ujira mdogo.

Wahamiaji hao walilazimishwa kuishi katika mazingira magumu hasa kwenye magofu, vibanda na viwanda ambavyo havifanyi kazi tena. Kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Italia linalopambana na usafirishaji haramu wa watu waliwahamisha wahamiaji hao hadi kwenye makambi maalumu katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.