Muongozo mpya kuhusu dawa za watoto watolewa na WHO na UNICEF

30 Aprili 2010

Mashirika mawaili ya Umoja wa Mataifa yametoa muongozo mpya kwenye wavuti wa wapi unaweza kupata dawa zilizotengenezwa kwa ajili ya watoto.

Muongozo huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, unaweza kuzuia vifo vya watoto milioni tisa kila mwaka vitokanavyo na maradhi ambayo ynaweza kuzuilika na kutibika.

Mkurugenzi wa madawa na sera wa WHO Hans Hogerzeil amesema kuimarisha upatikanaji na uwezo wa kupata dawa za watoto bado ni tatizo kubwa kwa watoto wengi walioko kwenye nchi masikini.

Muongozo huo ambao pia unaelezea wapi pa kupata dawa na bei zake kwa baadhi ya dawa utawasaidia madaktari na mashirika kupata dawa muhimu aina 240 ambazo zitaokoa maisha ya watoto.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter