Mratibu wa UM wa masuala ya kibinadamu amezuru Kivu DRC

30 Aprili 2010

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura John Holmes ambaye yuko ziarani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , leo amezuru jimbo la Kivu ya Kusini.

Akiwa Kivu ametembelea kambi ya wakimbizi wa ndani iliyoko Mwenga takribani kilometa 80 kusini magharibi mwa mji wa Bukavu na kukutana na viongozi wa eneo hilo na wafanyakazi wa misaada.

Katika mkutano wao amesisitiza kuwalinda raia, kusambaza misaada ya kibinadamu na kuahakikisha misaada hiyo inawafikia walenga ni jukumu la serikali .Kivu Kusini ni kitovu cha mapambano baiana ya jeshi la serikali na wanamgambo wa Kihutu kutoka Rwanda wa FDLR. Kivu hivi sasa kuna wakimbizi wa ndani milioni 1.4.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter