Ban Ki-moon amesisitiza jukumu la UM katika vita dhidi ya silaha za nyuklia

29 Aprili 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefafanua jukumu muhimu la Umoja wa Mataifa la kutafuta suluhu ya kudumu na ushirikiano ili kukabiliana na tishio la silaha za nyuklia.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la kimataifa la International Herald Tribune, Katibu Mkuu amesema hamasa inaongezeka kote duniani ya kuachana na silaha za nyuklia. Ametaja hatua ya matumaini ya hivi karibuni ya Marekani kutangaza kuacha kuzalisha silaha mpya za nyuklia na kutozitumia kwa kuzingatia mkataba wa kutozalisha nyuklia Nuclear Non-Proliferation Treaty.

Pia ametaja kitendo cha ushujaa kilichofanywa na Rais wa Marekani Barack Obama na wa Urusi Dmitriy Medvedev kutia saini mkataba mpywa uitwao START treaty wa kupunguza uzalishaji wa nyuklia. Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa leo umesimama katika eneo jipya la "ground zero" kwa ajili ya upokonyaji silaha za nyuklia kimataifa , na kwamba enero hilo si tena la majonzi bali la matumaini"

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter