Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu azisihi serikali na taasisi kusimama kidete kulinda haki za vyombo vya habari

Katibu Mkuu azisihi serikali na taasisi kusimama kidete kulinda haki za vyombo vya habari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameziomba serikali, mashirika yasiyokuwa ya serikali na watu kote duniani kutambua kazi muhimu ya vyombo vya habari na hivyo kulipa uzito suala la uhuru wa habari.

Katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni inayaoadhimishwa kila mwaka May 3, Katibu Mkuu amesisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni haki ya msingi ya binadamu.

Amesema japo haki hii iko katika mikataba ya haki za kibinadamu , kuna serikali na wale walio na nguvu ambao wanakandamiza uhuru wa vyombo vya habari.