Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu imezitaka pande hasimu Nepal kuzuia ghasia

Ofisi ya haki za binadamu imezitaka pande hasimu Nepal kuzuia ghasia

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imezisihi pande hasimu nchini Nepal kuzuia ghasia kufuatia kundi linalofuata siasa za Kimao kutangaza kuandamana siku ya Jumamosi.

Richard Bennet mwakislishi wa ofisi ya haki za binadamu nchini Nepal ameitaka serikali ya nchi hiyo kuzingatia haki za msingi za binadamu na pia uhuru wa kujieleza.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mjini Kathmandu Bennet amewasihi waandaaji wa maandamano hayo kuhakikisha kuwa wataheshimu sheria na haki za watu wengine kwa kufanya maandamano ya amani na utulivu.