Skip to main content

UNESCO yataka uchunguzi dhidi ya kifo cha mwandishi habari Cameroon

UNESCO yataka uchunguzi dhidi ya kifo cha mwandishi habari Cameroon

Mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ametaka uchunguzi ufanyike wa kifo cha mwandishi habari aliyekuwa jela nchini Cameroon.

Mwandhishi huyo ambaye alikuwa mhariri wa gazeti la kila siku Cameroon Express, Ngota Ngota Germain alikuwa rumande katika jela ya Kondengui mjini Yaunde kwa karibu miezi miwili sasa. Kwa mujibu wa shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka Germain alikuwa na matatizo ya athma na ugonjwa wa moyo, na alikuwa rumabe kwa madai ya udanganyifu.

Mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova ameelezea hofu yake juu ya kifo hicho na kusisitiza ufanyike uchunguzi. Serikali ya Cameroon kwa upande wake imeshathibitisha kuwa itachukunga kifo cha mwandishi huyo.