Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Tajikistan insema tatizo la polio kwa watu wake ni kubwa

Serikali ya Tajikistan insema tatizo la polio kwa watu wake ni kubwa

Wizara ya afya nchini Tajikistan imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani WHO kuhusu visa 171 vya polio.

Uchunguzi wa maabara nchini humo umebaini kuwepo kwa virusi vya polio type 1 kwa watu 32 na wengine 139 bado wanachunguzwa. Kati ya wilaya 68 nchini humo wilaya 24 zimeathirika na ugonjwa huo. Hadi sasa watu 12 wameshafariki dunia, 10 wakiwa ni watoto wa umri wa chini ya miaka 15 na wawili ni watu wazima.

Uchunguzi huo pia umethibitisha kwamba aina ya virusi vya polio vilivyopatikana Tajikistan ni sawa na vile vilivyopo Uttar Pradesh nchini Idia. Jopo la wataalamu wa WHO waliko Tajikistan wamekuwa humo tangu tarehe 16 ya mwezi huu kuchunguza kuzuka kwa polio na kuisaidia serikali katika msaada wa kiufundi kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.