Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA kusaidia watoto wa Palestina kusoma kwa kutumia compyuta

UNRWA kusaidia watoto wa Palestina kusoma kwa kutumia compyuta

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada na kazi kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA linasema umefika wakati wa kuwasaidia watoto wa Palestina kupata elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

UNRWA kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali yaani NGO wamewanzisha mradi utakaowasaidia watoto kupata fursa ya elimu kwa kutumia kompyuta.

Mradi huo ujulikanao One Laptop One Child (OLPC) utatoa kompyuta aina ya laptop kwa kila mtoto na utawanufaisha watoto wa wakimbizi wa Palestina wapatao nusu milioni ifikapo mwaka 2012.

Philipo Grandi ni mkurugenzi wa UNRWA