Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM ameanza ziara DR Congo

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM ameanza ziara DR Congo

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa John Holmes ameanza ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Homes ambaye atakuwa katika ziara ya siku tano nchini humo atazuru majimbo matatu yaliyoathirika vibaya na vita, ikiwemo Kivu ya Kusini, Oriantale na Equateur. Wakati wa ziara yake atajadili na kubainisha masuala muhimu ya kibi

nadamu ya kupewa kipaumbele na hatua za muhimu za kuchukuliwa hasa katika kuimarisha usalama na matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu. Suala la kuwalinda raia pia lipo katika ajenda.

Congo ni moja ya nchi iliyo na matatizo makubwa ya kibinadamu, na inakadiriwa kuwa watu takribani milioni mbili ni wakimbizi wa ndani kutokana na vita na wote hao wanahitaji msaada.