Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amesema kutokomeza silaha za kemikali ni tunu kwa waathirika

Ban amesema kutokomeza silaha za kemikali ni tunu kwa waathirika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuimarisha mkataba wa kimataifa wa kupinga silaha za kemikali kama njia ya kuwaenzi waliopoteza maisha yao kwa silaha hizo.

Katika ujumbe wake wa siku ya kuwakumbuka waathirika wa silaha za kemikali inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 April amesema kuimarisha mkataba wa kupinga silaha hizo ndio njia pekee ya kuwakumbuka na kuwaenzi waliopoteza maisha.

Ameongeza kuwa tuzikumbuke pia familia za wahanga hao tukishirikiana kuifanya dunia kuwa huru na silaha hizo. Mkataba wa kupinga silaha za kemikali ulianza kutekelezwa miaka 13 iliyopita.