Tatizo la fistula ni kubwa miongoni mwa wanawake wa Darfur Sudan

28 Aprili 2010

Mtaalamu maarufu wa masuala ya wanawake amesema tatizo la fistula na vifo vya kina mama wenye umri wa kuweza kuzaa ni kubwa kwenye jimbo la Darfur Sudan.

Dr. Adam Saleh, ambaye amekuwa akiwasaidia wanawake kwenye jimbo hilo kwa miaka kumi sasa ameutaka mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID kuwasaidia wagonjwa wa fistula kwa kujenga kitengo cha upasuaji.

Akizungumza na Radio ya UNAMID amesema tatizo la fistula ni kitu kilichozoeleka Darfur kwa sababu wanawake hawawezi kupata huduma ya upasuaji inayotakiwa wanapopata matatizo wakati wa kujifungua. Dr. Saleh amesema yeye pamoja na madaktari wengine wanawasaidia wanawake wapatao 50 kila mwaka kwenye jimbo la Darfur.

Pia amesema kwamba kuwa wagonjwa 60 ambao wameshatibiwa na sasa wamepatiwa mafunzo kama wakunga na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya Darfur, lakini wanahitaji kulipwa ili kufanya kazi na jamii zao.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter