Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel

28 Aprili 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel ambaye pia ni naibu waziri mkuu Ehud Barak .

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel ambaye pia ni naibu waziri mkuu Ehud Barak . Mkutano wao umekuja wakati jumuiya ya kimataifa inaendelea na juhudi za kufufua mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina.  Afisa wa ngazi za juu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni ameonya kuwa hali bado iko njia panda baina ya pande hizo mbili kiasi cha kuzuia kuanza kwa mazungumzo ya amani.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na waziri wa ulinzi wa Isarel wamejadili matarajio ya kupiga hatua katika mchakato wa amani ya mashariki ya kati.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter