Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto nchini Niger wamepokea mgao wa kwanza wa chakula

Watoto nchini Niger wamepokea mgao wa kwanza wa chakula

Leo Jumatano watoto takribani 800 wenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi miezi 23 wamepokea mgao wa kwanza wa chakula.

Mgao huo wa mwezi mmoja ni sehemu ya chakula kitakachogawiwa kwa miezi minne katika kijiji cha Koleram jimbo la Zinder kusini mwa Niger. Mpango wa kugawa lishe hiyo unafadhiliwa na pmango w chakula duniani WFP, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa watoto UNICEF na mashirika 13 yasiyo ya kiserikali kama sehemu ya mpango wa serikali wa kukabiliana na upungufu wa chakula nchini humo.

Lengo la mradi huo ni kuwalisha watoto nusu milioni katika maeneo yanayokabiliwa na utapia mlo uliokithiri na kupindukia asilimia 15 inayoelezwa shirika la afya duniani WHO. WFP na UNICEF wanasema majimbo yote ya Niger isipokuwa Niamey,watapata mgao huo wa chakula.