Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ametoa wito wa kuongeza ufadhili katika teknolojia inayojali mazingira

Ban ametoa wito wa kuongeza ufadhili katika teknolojia inayojali mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesisitiza haja ya kuongeza ufadhili katika matumizi ya nishati ya tekinolojia inayojali mazingira.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya kundi la washauri wa masuala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, amesema maamuzi yanyofanywa leo kuhusu hatma ya nishati yatakuwa na athari kubwa kwa mazingira, maendeleo, ukuaji wa uchumi na usalama wa kimataifa.

Ban pia ameainisha kwamba zaidi ya watu bilioni moja na nusu wanaishi bila kuwa na umeme jambo ambalo linaathiri afya zao, elimu ya watoto wao na kuwanfanya wasalie katika umazikini.

Ban amesema uwezekano wa kupata nishati nafuu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi na kufikia malengo ya milenia ili kukabiliana na umasikini na kuimarisha maisha ya watu ifikapo mwaka 2015.