Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafasi kwa wasichana ni muhimu kwa mabadiliko katika jamii

Nafasi kwa wasichana ni muhimu kwa mabadiliko katika jamii

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watopto UNICEF kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha New School jijini New York, leo limefungua warsha kubwa kuhusu wasichana vigori.

Mada ya warsha hiyo ya kimataifa amabayo imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka mitano safari hii mada ni wasichana vigori ndio nguzo ya jamii. Warsha hiyo inawajumuisha wadau kama wanazuoni, mashirika ya maendeleo, sekta kibinafsi, watunga sera na maafisa kutoka umoja wa mataifa. Warsha hiyo itajadili nafasi ya wasichan vigori katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Idadi ya vijana vigori ulimwenguni ni theluti moja, na kati ya watu bilioni mbili waliochini ya miaka ishirini na nne, takribani nusu bilioni ni wasichana vigori. Mkrugenzi wa jinsia na haki wa UNICEF Elizabeth Gibbons amesema Wakati mwingi wasichana hawapewi nafasi sawa na wavulana katika ajira na masomo, kando na kuwa haki zao za kimsingi zinakiukwa kwa sababu ya sheria zinzowadhalilisha wasichana katika jamii.

Bi Gibbons ameongezea kuwa hadi pale wasichana vigori watakapopewa nafasi basi malengo ya milenia ya maendeleo hayatofikiwa ifikipo mwaka wa 2015. UNICEF iko katika mataifa na meneo 150 ikiwasaidia watoto kukuwa na kunawiri tangu wakiwa wachanga hadi watakapokuwa vigori.