Skip to main content

Ban ampongeza Malkia wa Jordan kwa kuzindua kitabu kipya cha watoto

Ban ampongeza Malkia wa Jordan kwa kuzindua kitabu kipya cha watoto

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amempongeza malkia Rania wa Jordan wakati wa hafla ya kuzinduliwa kwa kitabu chake cha watoto.

Kitabu hicho kinahusu marafiki wawili shuleni ambao walikosana kwa sababu ya mmoja kukibeza chakula cha mwenzake. Lakini baada ya kupelekwa kwenye ofisi ya mwalimu mkuu, marafiki hao walilazimishwa kila mmoja kuonja chakula cha mwenzake, na ndipo wakatambua kumbe chakula cha mwenzake sio kama alivyokidhania.

Bwana Ban amesema katika karne hii ya 21 kitabu kama hiki kinahitajika ili kufanikisha utengamano kati ya tamaduni tofauti. Kwa upande wake Malkia Rania amesema ni rahisi kutambua kitu ambacho ni kigeni kuwa ni duni, na kuongeza kuwa kwa kujaribu kujua kuhusu mila na desturi za wengine tutajifunza kitu kutuhusu kwamba ni sawa na utamaduni wa watu wengine.