Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ameikaribisha hatua ya kuachiwa huru walinda amani wa UNAMID

Ban ameikaribisha hatua ya kuachiwa huru walinda amani wa UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameikaribisha hatua ya kuachiliwa huru walinda amani wanne waliotekwa wiki mbili zilizopita Darfur Sudan.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo na msemaji wake , Katibu Mkuu amesema amefarijika kusikia walindamani hao wa mpango wa kimataifa wa kulinda amani Darfur UNAMID wameachiliwa huru. Amesema anathamini juhudi zilizofanywa na serikali ya Sudan kuhakikisha walinda amani hao wanne wanaachiliwa katika hali ya usalama.

Kwa mara nyingine Katibu Mkuu amesisitiza kwa pande zote umuhimu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wengine walioko Sudan kuwasaidia watu wa Darfur.

Walinda amani hao wanne ambao ni polisi kutoka Afrika ya Kusini , wanaminika kuwa katika afya njema lakini uchunguzi zaidi wa afya zao utafanyika. Ban pia ameishukuru serikali ya Afrika ya Kusini kwa mchango wake wa kuhakikisha wanaachiliwa.