Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS imeipongeza Uchina kuondoa vikwazo vya usafiri kwa wenye HIV

UNAIDS imeipongeza Uchina kuondoa vikwazo vya usafiri kwa wenye HIV

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limeipongeza serikali ya Uchina kwa kuondoa vikwazo vya usafiri dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV.

Habari hii imekuja wakati Uchina inajiandaa na ufunguzi wa maonyesho ya Shangai yaani Shangai Expo 2010 ambayo ni maonyesho ya kimataifa ayanayotarajiwa kuvutia mamilioni ya watalii kwa miezi sita ijayo.

UNAIDS inapinga vikali sheria zozote ambazo zinazuia watu kusafiri kutokana na hali yao ya kuwa na virusi vya HIV. Inasema vikwazo hivyo ni ubaguzi na havizuii maambuki wala kulinda afya ya jamii. Kwani watu wenye HIV wanaweza kuishi na kufanya kazi kama kawaida.