Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imekaribisha hatua ya wakimbizi wa ndanu kurejea nyumbani Sri Lanka

UNHCR imekaribisha hatua ya wakimbizi wa ndanu kurejea nyumbani Sri Lanka

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeikaribisha hatua ya serikali ya Sri Lanka ya kuwasaidia wakimbizi wa ndani kurejea nyumbani.

Hatua hiyo ilisita kwa wiki tatu kufuatia uchaguzi wa bunge na sherehe za mwaka mpya wa Tamil.

Wakimbizi hao wa ndani ni wale waliosambaratishwa na miongo kadhaa za vita na kulazimika kuzikimbia nyumba zao kaskazini mwa nchi hiyo.

Tangu kuanza shughuli hiyo wiki jana wakimbizi wa ndani 7000 wamerejea nyumbani katika wilaya za Kilinochchi na Mullaitivu ambazo zote zilishuhudia mapigano makubwa kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Tamil Tigers kabla ya kundi hilo kufurushwa mwaka jana.

Andre Mahecic ni msemaji wa UNHCR