Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa G8 watakiwa kutoa uzito kwa afya ya mama na mtoto

Viongozi wa G8 watakiwa kutoa uzito kwa afya ya mama na mtoto

Mawaziri kutoka nchi nane tajiri duniani G8 wanakutana Halifax kuamua masuala ya maendeleo ya kuyapa kipaumbele kwenye mkutano wa viongozi utakaofanyika mwezi Juni.

Mkurugenzi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran anasema hakuna jambo muhimu na la haraka katika malengo ya maendeleo kama afya ya mama na mtoto. Amesema hiyo ndiyo iwe ajenda, ni rahisi kuelewa kwa nini, kwani kila mwaka zaidi ya watoto milioni 3.5 wanafariki dunia kwa kukosa lishe bora, hii ni sawa na watoto 10,000 wanaopoteza maisha kila siku.

Ameongeza kuwa hakuna msingi wa malengo mengine ya maendeleo kama lishe ya mama na mtoto haitofanikiwa. Canada ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo wa G8 iko msitari wa mbele kupigania suala hilo.