Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi unahitajika kunusuru wanaokumbwa na njaa Niger:OCHA

Msaada zaidi unahitajika kunusuru wanaokumbwa na njaa Niger:OCHA

Mwezi huu wa Aprili Umoja wa Mataifa umezindua mpango wa msaada wa kibinadamu wa kukusanya dola milioni 190 kusaidia operesheni zake nchini Niger.

Watu milioni 7.8 au asilimia 58 ya watu wote wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Mpaka sasa ni asilimia 30 tuu ya fedha hizo ndio zimepatikana. Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu msuala ya kibinadamu OCHA anasema dola milioni 133 zaidi zinahitajika haraka kwa ajili ya kununua chakula na vitu vingine.

OCHA inasema athari za njaa hiyo tayari ni kubwa, watu wengi wanakimbia vijijini kwenda mijini, na mfumo wa elimu umeathirika .Elizabeth Brys ni msemaji wa OCHA