Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na mwakilishi wa Marekani wajadili amani ya Mashariki ya Kati

Ban na mwakilishi wa Marekani wajadili amani ya Mashariki ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi maalumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa wamejadili juhudi zinazoendelea za kuifanya Israel na Palestina kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya amani.

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na bwana George Mitchell pia wamejadili hali ya Gaza na pendekezo lililowasilishwa miezi kadhaa iliyopita na bwana Mitchell la Israel na Palestina kuanza mazungumzo yasiyo rasmi yatakayosimamiwa na Marekani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya msemaji wa Ban Ki-moon ,Katibu Mkuu amemshukuru bwana Mitchell kwa juhudi zake na mchango wa Umoja wa mataifa.

Kuhusu suala la Gaza Ban amemweleza bwana Mitchell kuwa kumekuwepo na hatua zilizopigwa tangu alipofanya ziara Gaza mwezi Machi ingawa bado juhudi zaidi zinahitajika na ameitaka Marekani kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.